HISTORIA YA SAID SALM BAKHRESA
N a Prof. Muyungi & Monica Mathias ''Nilishona viatu kariakoo, Nililala kibarazani''-- Bakhresa , Ndugu mwanafamilia kumbe kwenye maisha kila kitu kinawezekana, kamwe usimdharau Mtu, hata kama leo anafanya kazi ya chini kiasi gani! kwakweli, tumeamini mambo yanabadirika, mtu unayemcheka na kumsimanga leo kwenye tasisi / kiwanda baada miaka ndo atakuwa boss wako. huwezi amini Bakhresa miaka ya 1957 aliyeonekana masikini wa kupindukia mpaka akaamua kuacha shule akiwa na miaka 14 lakini leo 2020 watu zaidi ya 5,000,000 [Milioni 5] katika nchi 5 wanategemea makampuni yake ili kuendelea kuishi! Mpendwa mwanafamilia wa Visiontanzania sisi ndio tunaojali mafanikio yako, siku ya leo tumekuletea bilionea orijino wa kitanzania ambaye maisha yake yalikuwa magumu vibaya sana, yahani ambaye nyumbani kula ilikuwa bahati nasibu kwa miaka ya 1950, lakini kwa leo ni moja ya mashujaa 3 kati ya watanzania zaidi ya 59,000,000 (Milioni 59) Tanzania, ana makampuni zaidi...