MAMBO YALETAYO FURAHA YA KWELI MAISHANI
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh-kWU6aVHmlajVWogpIi9sUzbXnebxRJp3rCOUSr0Av9PaJ_2wyev3npPkBnDZhHsAltB1UpF4RlEh4PLB9k9eSZ6KFIV9A4Gl2Y5l9GikfDktzGEa30zfXWu_t4iPJvoAlDY3oigGiME/s320/IMG_20200510_132445.jpg)
MAMBO YALETAYO FURAHA YA KWELI N a Prof. Muyungi & Monica Mathias ''Dunia ni mapito'' Prof. Muyungi, Duniani kote kila mtu huishi mara moja tu hakuna mtu yeyote aliyewahi kufariki alafu akazaliwa tena, ukimuuliza mtu yeyote maana ya maisha uwezi kamwe kupata jibu moja ila kwa ufupi maisha yako yapo akilini mwako kwahiyo unavyo yaona ndivyo yalivyo,na unachowaza na kufanya ndicho kinayafanya maisha yako kuwa hivyo. unaweza kusema maisha magumu hamna hela lakini ukiangalia kwenye vyombo vya habari utasikia msanii fulani kanunua Ghorofa la Bilioni tatu yaani wakati wewe uko hoi hata milioni 10 ni ya kufikirika, kwa hiyo hatuwezi kuwa na maana MOJA ya maisha Katika makala ijayo tutakuonyesha thamani ya maisha yako, utajiri ulio nao, sababu za ushindi wako....n.k Furaha ndio msingi mkubwa wa maisha ya Mtu yeyote, na hivyo shughuli zote unazofanya lengo lake ni kupata furaha na sio vinginevyo mfano mtu anakuwa dactari ili afurahi, anakuwa injinia ili afurahi, ...