MAANA SAHIHI YA UBUNIFU
MSINGI WA KUWA MGUNDUZI N a Prof. Muyungi & Monica Mathias UBUNIFU ni kitendo cha kutumia njia mpya zilizo bora zaidi katika kutatua changamoto husika [yahani kujua ufanye nini? kivipi? na wapi?], na haimaanishi tu kuja na wazo au kitu kipya kaabisa, ila pia maana ya kutumia njia ya kawaida katika kufanya jambo na kuiongezea ubora zaidi na kuifanya kuleta matunda zaidi. ''Mama kati ya yai na kuku kipi kilianza? Rose aliuliza, mama akawa anawaza nikimwambia ni kuku ataniuliza mbona vifaranga wanatoka kwenye mayai? pia mama akafikiria nikisema ni yai ataniuliza mbona kuku ndo wanazalisha mayai? mama akakosa jibu akamwambia mwalimu atakufundisha. Stori hii inatuonyesha namna gani Rose alikuwa mbunifu anataka ajue kipi kinategemea kingine?ndugu msomaji vyivo hivyo kwenye maisha kuna vitu tunapaswa tujue ili tupate kupiga hatua zaidi mbele, Benjamin Ferdinandes aliwahi kusema " Maisha ya mtu ni chembe chembe ndogo za matukio amba...