Posts

Showing posts from February 8, 2021

Mwanamke anayehitajika kwa jamii ya leo

Image
MWANAMKE BORA N a Monica Mathias Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke yanatakiwa kumaanisha uhalisia, wanawake mashujaa wanapaswa kuishi maisha ambayo yanawatambulisha kama mfano wa kuigwa ili wanapozungumza na kufundisha mabadiliko wawe tunazungumza uhalisia wa maisha yao ambao unajengwa na haya yafuatayo; UVUMILIVU Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbali mbali yasiyotuvutia katika mahusiano yetu, mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi kama vile; chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko, manung’uniko, machafuko, kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako. Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo. UPENDO WA DHATI Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafiki kwa jamii inayomzu...