MAANA SAHIHI YA UBUNIFU
MSINGI WA KUWA MGUNDUZI
Na Prof. Muyungi & Monica Mathias
UBUNIFU ni kitendo cha kutumia njia mpya zilizo bora zaidi katika kutatua changamoto husika [yahani kujua ufanye nini? kivipi? na wapi?], na haimaanishi tu kuja na wazo au kitu kipya kaabisa, ila pia maana ya kutumia njia ya kawaida katika kufanya jambo na kuiongezea ubora zaidi na kuifanya kuleta matunda zaidi.
''Mama kati ya yai na kuku kipi kilianza? Rose aliuliza, mama akawa anawaza nikimwambia ni kuku ataniuliza mbona vifaranga wanatoka kwenye mayai? pia mama akafikiria nikisema ni yai ataniuliza mbona kuku ndo wanazalisha mayai? mama akakosa jibu akamwambia mwalimu atakufundisha.
Stori hii inatuonyesha namna gani Rose alikuwa mbunifu anataka ajue kipi kinategemea kingine?ndugu msomaji vyivo hivyo kwenye maisha kuna vitu tunapaswa tujue ili tupate kupiga hatua zaidi mbele, Benjamin Ferdinandes aliwahi kusema "Maisha ya mtu ni chembe chembe ndogo za matukio ambazo zina namna yake ya kipekee kuzipangilia ilikuleta picha kamili'' [human life is a collection of numerous small particles which possess a unique pattern to form a clear picture]
kitu cha kipekee katika kila maisha ya mtu ni namna ya kufikiri na hapa ndipo hoja ya ubunifu hutokea, namna akili zetu zinavyo chakata kitofauti ndivyo ubunifu wetu unatofautiana, Mwanasaikolojia Dr. Lakey Jake aliwahi kusema ''Tofauti kubwa kati ya Binadamu na nyani ni kwamba binadamu ana AKILI na nyani ana SILIKA'' [The major difference between man and monkey is that a man has INTELLIGENCE but a monkey has INSTINCT] [ona ushaidi katika zaburi 103:20] kutokana na utofauti wetu katika matumizi ya akili ndio inatufanya kuwa tofauti katika ubunifu hata katika hali za maisha.
AKILI ni kipawa huru alicho nacho binadamu kinacho muwezesha kufikiri, kujifunza, kupanga, kuwasiliana na kutatua matatizo, hivyo kipawa hiki kinampa ufahamu unaoweza kumwonesha wema na ubaya na kufanya maamuzi, na kipawa hiki anacho binadamu pekeake kati ya wanyama na wadudu wote.
Ambapo wanyama na ndege, hutumia silika, SILIKA ni uwezo finyu tabuzi wa kutunza kumbukumbu chache ni uwezo wa kurithika unamsaidia mnyama au ndege kupata mahitaji yake, uwezo huu umfanya mnyama kutenda jambo bila utashi yahani ufanya vitu kwa hisia, hamu, mwenendo, ulinganishaji hapa mnyama hana uwezo wa kufikiri na hivyo mtumia silika awezi kubuni chochote. Ndio maana unaweza kumkuta mbuzi anakula mazao shambani kwako ukampiga ukamvunja mguu alafu kesho yake ukamkuta tena!
Ubunifu ndio chanzo cha kila kitu Duniani na nje ya Dunia, hivyo hatuna budi kusema Mungu ndiye Mbunifu mkuu na aliye achilia uwezo wa kubuni katika akili ya binadamu, kadiri binadamu anavyo kuwa mbunifu zaidi ndivyo anajitengenezea nafasi kubwa ya kuwa tajiri [yaani kuwa na kitu chochote anachohitaji kwa wakati] hivyo kitendo cha mtu kujiusisha na mambo ya kiubunifu anakuwa anaitangazia nafsi yake utajiri unao kuwa unatarajiwa.
UGUNDUZI Ni neno ambalo wengi hupenda kulitumia kumaanisha UBUNIFU. maneno haya yanaelekeana lakini yana maana tofauti kabisa UGUNDUZI : Ni kitendo cha kuwa na wazo na kulileta wazo katika uhalisia wa kitu kinacho hisika kupitia milango ya fahamu, Ubunifu ndio msingi wa Ugunduzi yaani kupitia ubunifu unajua ufanye nini? na ufanye vipi? kwa kutumia nini? na lini? (Ubunifu/creativity ni wazo, Ugunduzi/ Innovation ni wazo katika uhalisia) sasa unapokuja kwenye ugunduzi ndipo unazitumia hoja za ubunifu na kuja kitu kipya yaani Kugundua.
Kwahiyo katika UBUNIFU unapata mbinu hoja, mbinu, misingi, mawazo ya kutumia ili kupata jambo fulani, lakini katika UGUNDUZI unatumia mbinu ulizobuni na Kuweka kitu katika Uhalisia.
Tunaamini kila mtu afanikiwe lazima awe na ubunifu katika kutumia akili yake na kuelekea ndoto yake hivyo kila binadamu hana budi kufahamu kiundani zaidi mbinu kuu za ubunifu ili afanikiwe kugundua kitu chcochote anachotaka.
Soma hapa Mbinu za Kuwa Mbunifu Kitaalamu zaidi
Asanteni sana kwa kuwa nasi, tunakutakia utekelezwaji mwema. #visiontanzania
Comments
Post a Comment
Thanks for Commenting at Visiontanzania, Please Share These useful materials to your friendsππ
Asante,
Regards,
System Administrator,
Visiontanzania,
+255747787796
+255673787796