MFAHAMU FLAVIANA MATATA MPAMBANAJI TOP

MPAMBANAJI  MSHINDI

Na Prof. Muyungi & Monica Mathias

''Mstakabali wa maisha ya mtu huwa ni kwa namna gani umelelewa''   Ni huzuni sana Flaviana Matata alimpoteza mama ake mpendwa katika hajali ya MV BUKOBA iliyotokea 1996,  kwakweli hili lilikuwa pigo kubwa sana kwake na ilionekana ingekuwa sababu ya kupoteza matumaini kwenye maisha kwa hiyo alilelewa na baba tu na kuyakosa mapenzi ya mama.
alisoma chuo cha Arusha [Arusha Technical College] Aliwaza kuwa injinia lakini kwa sababu ya maisha magumu mwaka 2007 alianza umisi na ndoto ya uinjinia ikafa.
iliwashangaza sana watu kuona mtu aliyewaza uinjinia anaanza umisi lakini ndiyo iliyo kuwa ndoto yake kubwa tangu zamani.

Visiontanzania imekuletea maisha ya mwanadada hasa kwa wapambanaji wote wanaotaka kufanikiwa , kuona ni namna gani mafanikio ya kweli yanaweza kuja, mwanadada huyu awe mfano wa kuigwa na kila mtu apate kujipongeza kwa kutoa mchango wa maendeleo nchini kwake.
             
Flaviana Matata ni mwanamitindo kutoka nchini Tanzania alizaliwa mnamo tarehe 9 June, 1987,  ni miongoni mwa wanamitindo maarufu wa Tanzania na duniani kote., Mwanadada huyu amekuwa katika maisha ya magumu sana ambayo yangeweza kumkatisha tamaa na kuweza kupoteza  ndoto zake lakini hakuweza kukata tamaa hata siku moja kwani alitamani sana kufikia na kuishi ndoto yake.

Mnamo mwaka 2013 jarida la fobes la afrika  liliandika kuwa ni miongoni wanamitindo ambao kwa sasa wanaingiza kipato kikubwa Afrika kati ya wanamitindo saba, lakini pia mwaka jana (2019) aliweza kuandikwa na mtandao maarufu duniani wa okay.com kuwa ni miongoni mwa wanawake 100 wenye ushawishi zaidi barani afrika, lakini pia mrembo huyu kutoka mkoa wa shinyanga nchini Tanzania ameweza kufanya kazi na makampuni mbalimbali duniani kote nah ii imepelekea kuwa    maarufu na watu wengi kumfahamu kwa namna moja ama nyingine.
Flaviana akiwa na Rais wa Marekani  Donard Trump baada ya kuwa mshindi

Flaviana Matata amefanikiwa kufanya kazi na kampuni za The Lions nchini Marekani, Next Model Management ya ufaransa na uingereza, Boss Models ya Afrika kusini pamoja amefanya kazi na Sight Management Studios ya uhispania. Mwanadada huyu mara kadhaa huwa anapenda kuwaambia wadada wote wanaohitaji kupambana kufikia ndoto zao Kwamba ‘’hakuna alisema itakuwa rahisi , bakia kwenye kile unachoamini, fanya kazi kwa bidii na kuwa myenyekevu’’.
Mwanamitindo Flaviana akifurahia kazi ya kupambana kwake
Kwa sasa hapa nchini Tanzania mwandada huyu mbali na kuwa mwanamitindo pia ni mjasiriamali anajishughulisha na umiliki wa bidhaa zenye lebo ya lavy ambazo ni rangi za kupaka kucha za mikononi pamoja na taasisi ya Flaviana Matata Foundation ambayo inafanya kazi za kijamii katika kuhamasisha mabinti wadogo katika elimu, kupambana na kuamini katika vipaji vyao.
Flaviana  mpambanaji akiwa Marekani

Hakika kupitia Makala hii fupi juu ya mwanadada flaviana matata ambaye ni mwanamitindo ni mjasiriamali tunaweza kuona ni namna gani mafanikio hayapatikani kwa urahisi kiivo hivyo inatuhitaji kuwa watu wa kujituma sana ili kuweza kufikia malengo ambayo mtu anakuwa nayo katika maisha yake.

Flaviana alikutana na changamoto nyingi sana katika harakati za upambanaji lakini hatimaye ameweza kuwa mtu mkubwa sana Duniani, hivyo kupitia hapa anatuonyesha namna gani ametoa mchamgo wake mkubwa sana katika kukuza vipaji vya wanawake wengi Africa lakini pia dunia imemuweka kwenye listi ya wanawake 100 duniani wenye ushawishi mkubwa Duniani kumbuka duniani kuna watu zaidi ya bilion 7.7 yaani 7,700,000,000.

USHINDI HAUJI KWA BAHATI NASIBU TUJITAHIDI KUPAMBANA USIKU NA MCHANA, HAKUNA LISILO WEZEKANA.


Comments

Post a Comment

Thanks for Commenting at Visiontanzania, Please Share These useful materials to your friendsπŸ™ŒπŸ˜…
Asante,
Regards,
System Administrator,
Visiontanzania,
+255747787796
+255673787796

Popular Visiontanzania Posts

KIJANA MIAKA 18-35 USIKOSE HII

ACADEMY MEMBERSHIP ONLINE APPLICATION For VISION ENTREPRENEURSHIP ACADEMY

MENU

NGUZO KUU 8 ZA MAFANIKO KATIKA JAMBO LOLOTE

HISTORIA YA SAID SALM BAKHRESA

MAMBO YALETAYO FURAHA YA KWELI MAISHANI

FUNZO KUU LA KUFANIKIWA ATOA JACK MA

NJIA RAHISI YA KUISHI NDOTO ZAKO