NJIA RAHISI YA KUISHI NDOTO ZAKO
ISHI NDOTO ZAKO LEO
Na Prof. Muyungi & Monica Mathias
Watu wote Duniani uwa na mawazo tofauti tofauti, na hivyo watu huwa na matamanio ya kumiliki vitu fulani fulani, au kuwa katika vyeo na hali fulani, mfano mtu anaweza kuwa na matamanio ya kuwa mwanamziki mkubwa, kuwa kiongozi mkubwa, kumpata mchumba mwema, kumiliki magari ya kifahari, kuwa na nyumba nzuri, kuwa saidia watu wasiojiweza, kuwa na mpenzi mwaminifu n.k
chini ya 15% ya watu wote duniani, ndio walioweza kuwa na matamanio ya vitu mbali mbali vikubwa na hatimaye wakayafikia matamanio yao yahani NDOTO zao kwa wakati sahihi, ila watu walio wengi duniani matamanio yao huyafikia kwa taabu sana na wengi wao huishia katika matamanio tu, kwa sababu ya kushindwa kujua nini la kufanya na namna gani ya kufanya na wakati gani, na hivyo hiyo kuwa sababu ya watu wengi kushindwa kufikia ndoto zao.
Ndugu, Visiontanzania imekuletea njia kuu tatu ambazo ukiweza kuziishi utaweza kufikia ndoto zako mapema sana kwa wakati bila maangaiko makubwa, karibu kushikiana nasi tunao jari mafanikio yako katika kufikia ndoto zako.
NJIA KUU 3 ZA KUFIKIA NDOTO ZAKO
1. MWONEKANO WAKO KWA WATU
Siku zote tambua, ukitaka kufanikiwa katika jambo lolote lazima uwe tayari kuishi vizuri na watu, na hivyo kuna watu wa aina tofauti tofauti yahani kila mtu anamtazamo wake tofauti na mwingine.
Kuna msemo unasema "Kama wewe unajua u wa thamani basi ishi kithamani sio kimazoea" ikiwa na maana kwamba kama akilini mwako kama unaona una mawazo yakufanya vitu vikubwa yaani una ndoto kubwa, basi ishi kadiri ya ukubwa wa ndoto zako mbele za watu.
![]() |
Mfano kama unataka kuwa injinia jitengenezee mfumo wa maisha ya kiinjinia, vivyo hivyo kama unataka kuwa kiongozi mkubwa watu anza kuishi vema na watu wote ukiwa mfano wa kuigwa, kama unataka kuwa Dactari kuwa na mfumo wa tabia katika maongezi na matendo kama dactari, kama unataka kuwa mfanya biashara mkubwa jifunze namna ya kubana matumizi na kutengeneza faida kubwa kwenye mambo madogo madogo. Mtu ataanza kuwa Fulani, ikiwa atakuwa na sifa kamili za Fulani kumbe utakapo anza kuishi ndoto yako kimwonekano ni njia rahisi yako kufikia ndoto yako halisi kwa wakati.
Mwonekano wako mbele za watu, ni pamoja na unavyo vaa, unavyo suka, unavyo nyoa, unavyo kaa, unavyo tembea, unavyotembea, unavyoongea, unavyo tokezea kwa watu n.k vitu hivi vina mchango mkubwa katika kuelekea katika ndoto zako, ni jambo la ulazima kabisa kutambua tamaduni za jamii unapoishi ili ujue mahali gani kuna utaratibu gani,,,
![]() |
Risking is a vital part of great success |
Unavyoonekana ndiyo watu wanakuchukulia na ndivyo wanatengeneza picha yako akilini mwako,vilevile wataweza kukuongelea walivyo kuona, hivyo basi moja ya njia ya kuishi ndoto zako ni kujitahidi kuwa na mwonekano sahihi kadri ya maono ya ndoto zako na hapo utajitengenezea picha [image] nzuri kwa watu na wataweza kukusapoti na kukuwezesha kufikia malengo yako.
2. MATENDO UNAYOFANYA
Kipengele hiki kinaonyesha namna gani unaonyesha uhalisia wa kuelekea ndoto zako? na hapa ndipo watu uwa makini sana na kukuchunguza,
![]() |
Ili ufikie ndoto zako lazima ushirikiane na watu hivyo basi huna budi kuhakikisha matendo yako yanakuwa na uhalisia na kile unachokitafuta, ukifanya matendo hasi usitegemee kupata matokeo chanya, watu watakuamini kadiri yaa matendo yako na watakuongelea hivyo hivyo unavyotenda mfano, mzururaji, mwongo, mbishi, mtaratibu, mpole, anawahi , ana adabu n.k
Matendo yako uonyesha unachokifikilia, hivyo fikra zako uonyesha utu wako na maono yako katika maisha] Jitahidi kuchunga matendo yako, yanamaana sana katika kufikia ndoto zako, usipende kuishi maisha ya kuigiza, hilo litakukwamisha na utakosa sapoti kutoka kwa watu katika jitihada za kuelekea ndoto zako.
![]() |
Mtu anayeongea tu bila matendo ni sawa na mtu aliye sinzia huku akiota tofauti yao mmoja amesinzia mwingine hajasinzia |
3. MANENO YAKO
Watu wengi hudhani kuongea sana ndio kujua vitu vingi, na ndio kuongea ukweli, lakini sivyo kabisa....Ni muhimu sana ili kufanikiwa kujua unaongea nini kwa nani, kivipi,na lini,,,hii itakusaidia kuweza kuishi vema na watu wote. maneno mengi kwenye mazungumzo sio kuwa na hoja nyingi kubwa, ilaa mazungumzo mazuri ni yale mazungumzo yenye maneno machache, yakiambana na mfano na udhibitisho
Kadiri ya saikolojia mda mrefu sana wa mtu kukuelewa vizuri kwa unacho mwambia ni dakika 40, mda huo ukipita bila kupumzika grafu ya msikilizaji huanza kushuka na ikifika dakika 80 msikilizaji uanza kuacha kukufatilia na anaweza kusinzia
kutokana na hii ndio maana walimu na waubiri hujitajidi kutengeneza mifano mingi na vichekesho vingi ili kuwavutia wasikilizaji kisaikolojia.
Maneno unayoongea ndiyo yatakuletea marafiki wazuri au wabaya, kumbuka maneno hugawa watu, ni msingi sana kuhakikisha unafahamu ni wakati gani wa kuongea na wakati gani sio wa kuongea, pia kukaa kimya nayo ni moja ya njia sahihi ya kuishi ndoto yako.
![]() |
Unapofanya maongezi ni muhimu sana kupunguza maneno yako iwezekanavyo na kuwa sahihi mwenye kueleweka zaidi, kuongea sana sio kuwa na pointi nyingi, kumbuka maneno unayo yaongea ndio watu wananasa na kutengeneza picha yako vichwani mwao hivyo ikitokea watu wastaarabu wakasikia unaongea maneno ya ajabu ama matusi watakuona kuwa wewe ni mtu usiye na adabu na wakati mwingine hawatoweza kukusaidia na hivyo kukwama kutaanzia hapo.
Unapo fanya mazungumzo safi utapata watetezi, kwa kile kipindi watu wabaya watakapokuongelea vibaya bila wewe kuwepo mahali hapo pia utapata watu watakao kuunga mkono katika juhudi zako za mafanikio kwa maana wana picha nzuri ya maono yako kichwani
Unapo fanya mazungumzo safi utapata watetezi, kwa kile kipindi watu wabaya watakapokuongelea vibaya bila wewe kuwepo mahali hapo pia utapata watu watakao kuunga mkono katika juhudi zako za mafanikio kwa maana wana picha nzuri ya maono yako kichwani
Asanteni sana kwa kuwa nasi, tunakutakia utekelezwaji mwema. #visiontanzania
Comments
Post a Comment
Thanks for Commenting at Visiontanzania, Please Share These useful materials to your friendsππ
Asante,
Regards,
System Administrator,
Visiontanzania,
+255747787796
+255673787796