MAMBO YALETAYO FURAHA YA KWELI MAISHANI

MAMBO YALETAYO FURAHA YA KWELI

Na Prof. Muyungi & Monica Mathias

''Dunia ni mapito'' Prof. Muyungi,  Duniani kote kila mtu huishi mara moja tu hakuna mtu yeyote aliyewahi kufariki alafu akazaliwa tena, ukimuuliza mtu yeyote maana ya maisha uwezi kamwe kupata jibu moja ila kwa ufupi maisha yako yapo akilini mwako kwahiyo unavyo yaona ndivyo yalivyo,na unachowaza na kufanya ndicho kinayafanya maisha yako kuwa hivyo. unaweza kusema maisha magumu hamna hela lakini ukiangalia kwenye vyombo vya habari utasikia msanii fulani kanunua Ghorofa la Bilioni tatu yaani wakati wewe uko hoi hata milioni 10 ni ya kufikirika, kwa hiyo hatuwezi kuwa na maana MOJA ya maisha Katika makala ijayo tutakuonyesha thamani ya maisha yako, utajiri ulio nao, sababu za ushindi wako....n.k

Furaha ndio msingi mkubwa wa maisha ya Mtu yeyote, na hivyo shughuli zote unazofanya lengo lake ni kupata furaha na sio vinginevyo mfano mtu anakuwa dactari ili afurahi, anakuwa injinia ili afurahi, anakuwa mkulima ili afurahi, anakuwa mwanajeshi ili afurahi......chakushangaza mtu pia anakuwa gaidi ili afurahi, anakuwa mchawi ili afurahi, anakuwa mwizi ili afurahi, kwa kusema hivyo kumbe kila shughuli unayofanya lengo lake ni kupata furaha. Na hiki ni kitu ambacho kimejengeka akilini mwa watu hivyo wakati mwingine unaweza ukafanya shughuli bila kuwaza lakini hatima yake ni kutafuta Furaha.

Ndugu mwanafamilia wa Visiontanzania ni jambo lisilowezekana kabisa Kutenganisha maisha ya binadamu na Furaha,,msomi mmoja Prof. Muyungi, alisema ''Kiasi cha mda uliobakiza kuishi duniani kinaweza kukadiliwa kutokana na kipimo cha furaha uliyokuwanayo, uliyonayo na unayotegemea kuwa nayo'' [The Left  Duration for your life on the earth may possibly be determined by the Degree of  happiness you had, you have, and you expect to have], Nakumbuka bibi angu alikuwa ananisisitiza kucheka sana niwezavyo kila aliponipatia hadithi kumbe falsafa yake ilikuwa ndani ya furaha akiamini  mtu akiwa na furaha mda wake wote uenda anawezekano wa kuishi mda mrefu kwa amani, sikupingana na bibi lakini badae nimeona uhalisia kama utakavyoonyeshwa kwe makala ya SECRETS  OF LIFE.

Visiontanzania inakupenda sana na kujali mafaniko yako, Leo hii Prof. Muyungi & Monica Mathias wamekuandalia vitu muhimu sana ambavyo ndivyo muhimu kukutengenezea furaha ya Kweli kwenye maisha, tukiwa na lengo la kuwa pamoja nawe katika safari yako ndefu ya Mafaniko, makala hii imepatikana kutokana na ripoti mbalimbali za uchunguzi wa falsafa ya maisha ya Binadamu zilizofanywa na tasisi tofauti tofauti. Tunaamini utapata kitu cha kukujenga na kukuandaa kuwa na Furaha ya kweli kwenye Maisha.

AINA  ZA  FURAHA 

1. FURAHA YA KWELI : Hii ni Furaha ambayo ni ya kudumu, Furaha yenye misingi imara, ambayo hupatikana kutokana na kufanya vitu ambavyo ni vizuri mbele za watu, mfano ukisoma ukafaulu mtiahani, ukitoa ahadi ukaitimiza, Ukiwa na Mpenzi akakutimizia mambo yote kwa uaminifu, ukisema ukweli hata kwa kujitoa sadaka, Ukimsaidia asiye jiweza Mara zote Furaha ya kweli hutokana na kufanya kazi na watu kwa ajili ya mafanikio ya watu na kwa lengo jema.

2. FURAHA HASI:  Hii ni kinyume na Furaha ya Kweli, ni yaani mtu anajiona anafurahi wakati anateseka, ni kitendo cha kuidanganya nafsi kwamba anafurahi huku akiwa kwenye mateso ya ndani, dhamili yake inamsuta, mfano Kufanya wizi wa mali za rafiki ako, Kumsingizia mwenzako akafukuzwa kazi, Kura rushwa, kutengeneza vyeti feki, kumwongopea mpenzi wako, kukuso uaminifu kwa anayekuamini yahani matendo yote hasi yako hapa,,,,,,hapa sio kuzuri kwa ajili yako.


MISINGI  YA  FURAHA  YA KWELI

1. KUMJUA NA KUMTUMIA MUNGU [ SUPREME POWER AUTHENTICATION ] 40%

Mtaalamu wa Elimu ya Theolojia [knowledge about God] Pope John Paul II aliwahi kusema ''hapana kabisa kitu chochote chenye uwezo wa kuwepo bila kitu kisababishi, na hicho kisababishi ndicho tuitacho  Nguvu kuu Ya Asili yaani MUNGU'' [ It is automatically purely impossible for something to exist without a causative agent, and that agent is what we call Super Natural Power meaning GOD'' 


Hakika Mungu ndiye mwalishi wa kila kitu, yeye ndiye mwanzo na mwisho wa vitu vyote na ndo aweza amuru  chochote kitokee! Hivyo hata maisha tuliyo nayo tumepewa kutoka kwa Mungu, Utajiri ulionao, Elimu uliyo nayo, kazi uliyo nayo, Uongozi ulionao, Heshima uliyo nayo vyote vimetoka kwa Mungu!.......hata mtu anayepata kitu kwa njia isiyo rasmi Mungu kamuona.

Ili upate Furaha ya kweli maishani ni jambo kuu na la msingi, na umuhimu wake ni zaidi ya 40% za vitu vingine vyote muhimu ili kupata Furaha ya kweli.

Kumbe ili kuwa na Furaha ya kweli maishani ni jambo la lazima kufahamu kiundani uhalisia kuhusu Mungu, ingawa hatuwezi kumfahamu Mungu hata kwa 30% ila tukiziweza akili zetu na tumaini letu juu yake hii itakuwa njia bora na safi kabisa ya kufikia  Katika Furaha ya Kweli.

Kumtanguliza Mungu ni pamoja na kuzishika taratibu mbali mbali za dini yako pamoja na za serikali na jamii kiujumla, na kuishi vizuri na watu.

Ni muhimu Kumtanguliza Mungu katika Shughuli zote, Yeye atakupatia  baraka na neema tele za kukuongoza katika Maisha yote na utafanikiwa katika shughuli zako zote, Mungu ukimtanguliza katika maisha yako yote yeye atakusimamia na kukubariki na kuzibariki shughuli zako nawe utafanikwiwa na hiyo ndio itakuwa sababu ya Furaha yako.


2. KUJIFAHAMU NA KUWA SHUJAA [ AWARE SOME &  BRAVE ] 10%

Ni jambo la maana sana kujitafakari mara kwa mara, walau kwa mda mchache kwa siku ili kuona uwezo wako, na nguvu zako ziko wapi  Hii itakusaidia kufahamu kiu ndani zaidi jambo gani unaweza kulifanya kwa Uwezo wako na Ukafaulu ili kupata Furaha.

Mwana Mahesabu Michael Faraday alisema Ndani ya binadamu kuna utajiri unaoweza kubadilisha hali ya nchi nzima ndani ya mwaka mmoja, na utajiri huu utaweza kugundulika kupitia Tafakari mzamo [In a single person there is a great richness that may possibly change the whole country in the course of time of a year, but this richness can never be recognised in lack of Deep self Meditataion] Michael Faraday ni moja ya wanasayansi wabunifu zaidi s Duniani  na alitoa mchango mkubwa katika ugunduzi wa dainamo na motor vifaa muhimu katika karibia kila mashine unayoijua inatembea mfano mashine za kusaga, injini za magari, simu, compyuta, Redio n.k 

Faraday alikuwa mtu wa kawaida sana lakini alikuwa na tabia za kufanya tafakari binafsi yaani kuna kipindi alikuwa anakaa chumbani masaa 12 akifanya tafakari mpaka akaja na mchango mkubwa kwenye sayansi, alikuwa na furaha ya kweli kwa sababu walifurahia ugunduzi wake, hivyo basi na wewe ndani yako kuna utajiri mkubwa jitengenezee utamaduni wa tafakari utaweza kuja na ushindi mkubwa sana maishani, na hapa utaweza kuona jamii yako umeisaidia vipi kukua, usipite tu kama kivuli  katika kila jamii unapopitia tengeneza kitu cha tofauti chenye maendeleo

Siku zote jitengenezee mazingira ya ushupavu yaani usiteteleke, kama unajua jambo unalolifanya, na unajua ni jambo halali na jema kabisa kwako na kwa jamii husika basi hata ukikutana na changamoto kiasi gani....kamwe usisite kusogea mbele kwa imani na matumaini,  lakini kabisa inabidi kwanza ujiamini na usiwe tegemezi kwa yeyote, hata kama ni mzazi,mpenzi ama mwalimu [stand alone with God to speculate!].

Jitengenezee Uwezo imara 

Tafiti zinaonyesha watu wengi walio na furaha kubwa ni wale walio fanikiwa maishani, na hawa walikuwa mashujaa bila kujali ni mwanamke au la alipigana mpaka akaja na ushindi wa kishindo,,,Furaha ya kweli ni ile furaha unayopata kwa kupambana sio furaha ya vitu ulivyo pata bila uhalali.


3. KUTAMBUA  MARAFIKI WA KWELI [FULLY FAITHFUL FRIENDSHIP ] 25%

Marafiki zako ulionao ndio wanakufanya hali yako iwe hivyo, kamwe usiangaike kuwa na marafiki wengi wasio na faida, Robert Mugabe alisema '''Msichana anavyokuwa na marafiki wengi sana wa jinsia kiume kuliko jinsia yake huanza kupoteza Furaha bila yeye kujitambua'' [As a girl makes extraordinary boyfriends begins loosing her happiness in a gradual manner while unknowingly]Marafiki wanachangia kwa kiwango kikubwa katika mafanikio yako, marafiki ndio wanaweza kukuza au kuua kipaji chako,  ndio wanaweza kukujengea furaha ya kweli au huzuni wa kudumu, na hii inakuwa tatizo kwa watu walio wengi, mtaalamu wa saikolojia Prof. Muyungi, alisema Asilimia 80 ya watu wote duniani, kwenye matendo 10 wanayofanya matendo 4 tu ndio yanakuwa na uwezekano mkubwa wa uhalisia na mengine 6 yakiwa na chembe chembe za unafiki [80% of the world population, if one does 10 actions only 4 may base on the true reality while other more 6 actions must involve hypocratic elements]

Kupitia akili nzuri uliyo nayo huna budi kuitumia na kuwachambua marafiki zako ulionao na kuwaweka kwenye makundi ya kifalsafa na kujua rafiki yupi umwambie kipi na rafiki yupi umwambie hiki, maana sio kila ulicho nacho moyoni unaweza kumshirikisha yeyote akakusaidia unavyofikiri hapa Mwl. J.K Nyerere alisema ''Ukiona mtu anapenda kukufatilia sana katika mambo yako ya siri tambua huyo mtu uenda anakupenda sana na anataka akusaidie ufanikiwe katika kila kitu au huyo mtu anakuchukia sana anakupeleleza ili ajue nguvu yako iko wapi ili akuangushe,,,,lazima  awe sehemu moja wapo tu'' [If someone makes a deep speculations in all your personal matters/secrets he/she must be either highly loving you and wills to assist you in everything so as you may be successiful or may be highly hating you wants to know your strength so as to depress you into failure,,,no draw here]

Moja ya vitu vikubwa vya kujali katika kutengeneza mazingira ya furaha ya kweli ni lazima kuchunga sana ukaribu wako na marafiki zako, kuwa na msimamo katika mambo yako, na usimwambie kila rafiki siri zako, pia chunga sana ahadi unazo ziweka kwa marafiki zako usichokiweza usikiahidi, usicho na uhakika nacho usikiongee, usichokielewa usikiamini, usichokipenda kiseme ,unacho hitaji kiseme, unachokiogopa kiepuke.

Ukiambiwa kitu  tafuta sababu yake na thamani yake kisicho na faida kwa maisha ya badae achana nacho, unayempenda kuwa na sababu ya kumpenda hivi ndivyo vitu vitakavyo kutengenezea furaha ya kweli.

Johann Wolfgang von Goethe anasema ''Niambie rafiki zako, nikwambie wewe u nani.." "Tell me who your friends are, and I'll tell you who you are" Unapokuwa na ukaribu sana na mtu akili zenu huanza kuvutana na kujaribu kuunganika na kutengeneza fikra zenye kuelekeana, kama una rafiki anapenda mpira baada ya mda utajikuta unapenda mpira, kama unarafiki mpenda mambo maendeleo na uchumi baada ya siku utajikuta na wewe umeanza kuwa mpenda maendeleo na uchumi, lakini pia tabia hasi mfano rafiki yako kama ni mpenda mapenzi baada ya siku utajikuta huko,,,,,,,,na vile vile vile ukipenda wezi utakuwa mwizi, ukipenda mchelewaji utakuwa kama yeye haya yote yanatokea kulingana na mda...

Prof. Muyungi, hupendelea kuongea na vijana maneno haya ""Fanya kila kitu kwa mda wake, mahali pake, ukiwa na nia chanya, njia sahihi na lengo chanya'''[Do everything in its actual time, Exact Environment,Clear and Positive intention, exact person and In an acceptable manner ...hakika matendo yako yote yakiendana na utaratibu wa prof. schleiden Utajikuta mambo yanaenda bila kupinda kwenye maisha yako na utakuwa na Furaha ya kweli siku zote, utajiepusha na nafasi za kukwazana na watu, hautakuwa na migogoro na utaweza kujipatia Furaha ya kweli. 

Kuwa makini na rafiki uliye naye sio kila aonekanaye kuwa rafiki ni rafiki wengine wapelelezi na hapo Martin Ruther J.R alisema ''Urafiki ni muunganiko usioisha wa upendo wa moyoni kati ya nafsi moja na nyingine, kamwe urafiki hauwezi kuvunjika vinginevyo watu hao walikuwa hawapendani ila waliigiziana kitabia wakiongozwa na tamaa'''[Friendship is the endless Heartily love connections between one person and the other, Love friendship can never break up ,,,in reality once people say have broken love friendship in truely it means the two had never loved each other from the begining but were acting ]

Katika urafiki kuna vitu viwili Tamaa na upendo;;;;TAMAA ni  hisia fupi ya mtu juu ya mtu  akiwa anataka kummiliki na kuwa na uwezo wa kumtumia atakavyo na akisha kummiliki uzuri wake huona unapungua kila kukicha mwishoni uona  ni heri kutafuta mwingine, maana kadiri siku ziendavyo huona hamfai tena!;;;;;

UPENDO ni muunganiko usio na mwisho wa hisia ya moyo wa mtu mmoja na mtu mwingine thamani ya hisia zao uongezeka kila kukicha na mtu ueweza mwenzake kama yeye katika nafsi nyingine, yahani mwenzake akiumia yeye huumia zaidi, mwenzake akifanikiwa huona kama yeye mwenyewe amefanikiwa zaidi ndio maana ya upendo usio na mwisho...p.......Ni vigumu sana kumgundua mtu mwenye kukutamani kama huna elimu ya saikolojia, lakini vile vile mtu anayekupenda sio rahisi kumgundua kama huna historia huyo mtu na malengo ya huyo mtu lakini pia kama huna elimu ya saikolojia.

Ukiangalia vibaya unaweza kudhani mtu anayekutamani ndio anayekupenda, kwa sababu mtu anayekutamani kweli kweli anaweza kukufanyia vitu vikubwa na vya kushangaza mpaka akili yako ikastuka ukadhani anakupenda kumbe sivyooo! na mtu anayekutamani huanza akikujali sana na kukufanyia kila kitu cha kipekee lakini siku zinavyosogea tabia yake halisi uanza kuonekana na kuacha kukuthamini tena! mateso na usumbufu huanza baada ya kuwa amejihakikishia amekuteka na kukumiliki! 

katika kipindi cha kwanza cha mtu anayekutamani utapata furaha kubwa sana lakini kufika mwisho furaha hiyo huna tena! Mtu mwenye kutamani anakuwa na ushawishi mkubwa sana kuliko mwenye upendo wa kweli na 70% ya mahusiano yote yapo katika kundi hili 

Mtu anayekupenda ni mtu ambaye siku kadili zinavyosogea thamani yako kwake uongezeka na inafika kipindi anaona hawezi chochote bila uwepo wako, na mtu huyu yupo tayari kukwambia kitu chochote kinacho muhusu lakini pia kukupatia kitu chochote alicho nacho na watu hawa ndio wanaitwa wapendanao siku haiwezi kupita bila kukumbukana kwa maana nyingine Watu hawa wanakuwa wamoja katika nafsi mbili na hapo upendo unakuwa umekolea. Na hapo ndipo ilipo Furaha ya kweli,,,,,cha kushangaza sana inasemekana 30% ya watu wanaoanza mahusiano ndo wanaweza kufikia hatua hii.

kuwa maakini sana na marafiki, hao ndio wanaweze kukutengenezea furaha ya kweli lakini pia ndio wanaweza kukutengenezea huzuni ya kudumu siku zote!



4. KUMILIKI TARIFA NA MAARIFA [ KNOWLEDGE  &  INFORMATION ] 20%

Kipengele hiki ni muhimu pia, katika misingi ya kutengeneza furaha ya kweli kipengele hiki huchukua asilimia 20 [20%] ya mambo muhimu ili kuwa na Furaha ya kweli, kipengele hiki kinakusaidia namna ya kukaa na watu na kuchangamana nao.

Ukitaka kufurahi kwenye maisha lazima uwe na uwezo mzuri wa kukaa na watu, namna unavyoongea nao na vitu unavyoviongea kwao ndivyo vitajenga taswira ya Thamani yako kwao, kwahiyo ni wewe kuhamua watu kukuheshimu na kukupenda au la.

Ili uwe na uwezo mzuri wa kueleweka na kuaminika kwa watu chunga sana tarifa unazozitoa kwao namna gani unazitoa na kwa nani unazitoa. Prof. Honest Ngowi mtaalamu wa uchumi aliwahi kusema ''Heshima huja pale mtu unapojua unaongea nini, kwa nani na kivipi?'' [Respect comes when you know to whom you are talking, what you talk and how you talk'' ukiwa vizuri hapa utaweza kujijengea heshima kubwa ndani ya akili za watu hata usipokuwepo watakuongelea vizuri kwa sababu wana uhalisia uliowaonyesha.


















Jitengenezee utamaduni wa kutafuta tarifa, ili uwe na tarifa nyingi sana uwezavyo hii itakusaidia kuwa sahihi na wakueleweka katika mazungumzo yako ,,nilimskia Nape Nauye waziri wa Habari mstaaf Wa Tanzania alisema '''Video unazoziangalia,miziki unayosikiliza, na matangazo ya mitandaoni, stori unazopiga,vitu unavyo viwaza sasa ndivyo vitakufanya mtu wa namna gani badae'' [The videos you watch, the music you listen to, The posts you attend, and the stories you share are the ones will determine you future value and poition in the society

Tafadhali kama kweli unadhamilia kufanikiwa katika jambo lolote kuwa na tabia ya kujifunza kitu kipya kila siku, na sio lazima ujue vitu vikubwaaa! yaani vitu vya kawaida tu, kiasi kwamba siku ikiisha ujue leo nimejifunza maana ya neno jipya, maana ya neno flani, historia ya mtu fulani, chanzo cha jambo fulani, tabia ya  kitu, mbinu ya kufanya kazi, n.k mwisho wa jambo fulani yaani jitahidi kujifunza kila siku vitu vidogo vidogo,,,kwa mwezi utakuta umejifunza vitu vipya zaidi ya 20 na vitakusaidia katika kazi zako na utaweza kuwa na mafanikio zaidi na hivyo unajitengenezea mazingira ya kufurahi zaidi!

Kuna msemo wa kizungu unasema, No research no right to speak, yaani Bila utafiti wa jambo kamwe usiliongelee jambo, ikiwa utajikita katika kujiongezea taarifa mpya na ujuzi mpya utakuwa umekuza maarifa yako,utakuwa mtu wa watu , watu watakupenda, watakuomba ushauri kwasababu wanakuamini na kwa sababu unajua vitu vingi vyenye kuwajenga na kuwasaidia. 
Ndugu, msomaji  kumbuka furaha ya kweli hutoka kwa watu, ukiishi vema kwa kusaidia watu watu watakuona wa muhimu na wafaida kwao, ikitokea ukasemwa vibaya wale uliowasaidia watakutetea na utasikia kesi yako ilishaga isha  kumbe kipindi hicho utakuwa na furaha ya kweli.   
          
Asanteni sana kwa kuwa nasi, tunakutakia utekelezwaji mwema. #visiontanzania 


Comments

  1. Amina sana, Kwa kweli kuna vitu nilikuwa sijui ila sasa mmeniweka sawa, nashukuru

    ReplyDelete
  2. Kwakweli Maprofesa huwa mna mambo makubwa.... Ongera sana Mkurugenzi wa #SWIπŸ‡ΉπŸ‡Ώ Kwakweli kupia website ya kampuni lenu nimejifunza vitu vingi sana kuhusu suala zima la Mafanikio makubwa katika maisha..... Naombeni mnishirikishe fursa huko kwa #SWI Hatakama niwe mlinzi geitin nitashukuru sana wakuuπŸ™πŸ™ Mungu Mwenyezi awabariki #SWI Kazi yenu tunaionaπŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™

    ReplyDelete
  3. Replies
    1. Actually i have come to realize that we have alot to learn with alot to understand. Thanks SWI

      Delete

Post a Comment

Thanks for Commenting at Visiontanzania, Please Share These useful materials to your friendsπŸ™ŒπŸ˜…
Asante,
Regards,
System Administrator,
Visiontanzania,
+255747787796
+255673787796

Popular Visiontanzania Posts

KIJANA MIAKA 18-35 USIKOSE HII

ACADEMY MEMBERSHIP ONLINE APPLICATION For VISION ENTREPRENEURSHIP ACADEMY

MENU

NGUZO KUU 8 ZA MAFANIKO KATIKA JAMBO LOLOTE

MFAHAMU FLAVIANA MATATA MPAMBANAJI TOP

HISTORIA YA SAID SALM BAKHRESA

FUNZO KUU LA KUFANIKIWA ATOA JACK MA

NJIA RAHISI YA KUISHI NDOTO ZAKO