Kubadilika siri ya kufanikiwa

KUBADILIKA NI KUFANIKIWA 

Na Prof. Muyungi
 "Who ever is not ready to change, can never bring any positive change" ni kauli aliyoitoa Rais wa Marekani Barack Obama. 

Ukienda mtaani unauliza nini maana ya "Kubadilikautapata tafsiri kibao zenye mantiki inayaonyesha kuacha jambo moja na kuanza lingine, ni mara kadhaa utasikia kauli hizi "mwanangu siku hizi umebadilika.....", mfanyakazi amebadilika...", nimebadilisha...'' Hivyo sasa kubadilika kuna uhusiano wa moja kwa Moja kwenye kuachana na jambo moja na kuanza kushughulikia lingine.

Kubadilika: Ni kitendo cha mtu Kuwa na mtazamo tofauti katika jambo ambalo lilionekana la maana sana, na kuwa na Mtazamo chanya zaidi. 

Kuna aina mbili za mabadiliko
1. Mabadiliko Chanya: hiki ni kitendo cha mtu kuacha jambo baya na kuanzakufanya jambo jema au ni kitendo cha mtu kuacha jambo jema ambalo lina faida kidogo na kufanya jambo lenye manufaa zaidi na faida kubwa. Mfano Mfano Kuacha umbea, uzembe, matusi, kuacha kuhonga wanawake na kufanya uwekezaji.

2. Mabadiliko Hasi: hiki ni kitendo cha mtu kuacha jambo jema na kufanya jambo baya au kuacha jambo lenye faida zaidi na kufanya jambo lenye faida kidogo. Mfano kutumia fedha za mkopo kununua vyakula na nguo za kitajiri badala ya kufanya shughuli za kuongeza kipato.

Hakuna jambo litokealo bila sababu na hivyo kubadilika hotokea kwa sababu na mabadiliko ndio huwa chanzo cha mafanikio kwa Mtu Yeyote hii ikiwa na maana kwamba maendeleo makubwa kote duniani hutokana na utayari wa kubadilika na maendeleo makubwa katika uso wa nchi yametokana na watu ambao walikuwa tayari kubadilika. 

Kuna watu wanakuwa tayari kubadilika kwa wenyewe lakini pia kuna watu wanahitaji nguvu ya ziada ili kuweza kubadilika ...mfano Mwalimu hulazimika kutumia kiboko kumbadilisha mwanafunzi,,,serikali hutumia Magereza kuwabadilisha wananchi wasiotii sheria, Jeshini adhabu hutumika kuwabadilisha wanajeshi wasofata taratibu....

kubadilika sio jambo dogo kama tanavyo weza kulichukulia lina hitaji maandalizi na misingi imara, ikiwa ni pamoja na kujitambua na kuweka malengo imara kwenye maisha kwa kuwa na mtazamo chanya.

Mpendwa msomaji siku zote kuwa tayari kubadika, kuwa tayari kuwa na mtazamo mpya kwa shughuli zako, kuwa na tabia ya kuwa na mda wa kujitafakari hakika utagundua  fursa nyingi zilizo mbele ako, na hapo ndipo mafanikio yatatokea.,....Juhudi bila maarifa uchelewesha mafanikio pia kupambana bila kuwa tayari kubadilika huchelewesha mafaniko.

"A body in motion continues in motion unless acted by an external force" by Isaac Newton. Mtu anayetaka kufanikiwa sio mtu wa kungoja kusukumwa ndo abadilike ... Ukitambua thamani ya maisha yako utakuwa tayari kubadilisha mtazamo, hivyo kanuni ya mabadiliko sahihi inatakiwa kuwa kinyume na sheria ya mwendo ya Newton.

Kubadilika kunahitaji mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na falsafa ya hisabati ili uwezo kutumia akili za uwiano na fumulara mfuatano (logic) ili kutengeneza ramamani nzuri ya kuyafikia mafanikio na ndoto zako za maisha.

Badilika leo jenga maisha yako, Kuwa na mtazamo chanya kwa kila kitu , fanya kila kitu kwa sababu, chunga fikra, na jenga maarifa zaidi katika  juhudi na hayo yote yatakufikisha kwenye MAFANIKIO.

KUBADILIKA NDIO KUTAKUFIKISHA KWENYE MAFANIKO 

Comments

Post a Comment

Thanks for Commenting at Visiontanzania, Please Share These useful materials to your friendsπŸ™ŒπŸ˜…
Asante,
Regards,
System Administrator,
Visiontanzania,
+255747787796
+255673787796

Popular Visiontanzania Posts

KIJANA MIAKA 18-35 USIKOSE HII

ACADEMY MEMBERSHIP ONLINE APPLICATION For VISION ENTREPRENEURSHIP ACADEMY

MENU

NGUZO KUU 8 ZA MAFANIKO KATIKA JAMBO LOLOTE

MFAHAMU FLAVIANA MATATA MPAMBANAJI TOP

HISTORIA YA SAID SALM BAKHRESA

MAMBO YALETAYO FURAHA YA KWELI MAISHANI

FUNZO KUU LA KUFANIKIWA ATOA JACK MA

NJIA RAHISI YA KUISHI NDOTO ZAKO