LITANIA YA BIKIRA MARIA
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumieKristo utuhurumie
Bwana utuhurumieBwana utuhurumie
Kristo utusikieKristo utusikilize
Baba wa mbinguni Mungu,Utuhurumie
Roho Mtakatifu Mungu,Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu mmoja
Utuhurumie
Maria Mtakatifu,
Mzazi Mtakatifu wa Mungu,
Bikira Mtakatifu, Mkuu wa mabikira,
Mama wa Kristu,
Mama wa kanisa,
Mama wa neema ya Mungu,
Mama mtakatifu sana,
Mama mwenye usafi wa moyo,
Mama usiye na doa,
Mama usiye na dhambi,
Mama mpendelevu,
Mama mstaajabivu,
Mama wa shauri jema,
Mama wa Mwumba,
Mama wa Mkombozi,
Bikira mwenye utaratibu,
Bikira mwenye heshima,
Bikira mwenye sifa,
Bikira mwenye enzi,
Bikira mwenye huruma,
Bikira amini,
Kikao cha haki,
Kikao cha hekima,
Sababu ya furaha yetu,
Chombo cha neema,
Chombo cha heshima,
Chombo bora cha ibada,
Waridi lenye fumbo,
Mnara wa Daudi,
Mnara wa pembe,
Nyumba ya dhahabu,
Sanduku la Agano,
Mlango wa mbingu,
Nyota ya asubuhi,
Afya ya wagonjwa,
Makimbilio ya wakosefu,
Mfariji wa wenye uchungu,
Msaada wa Wakristu,
Malkia wa Malaika,
Malkia wa Mababu,
Malkia wa Manabii,
Malkia wa Mitume,
Malkia wa Mashaidi,
Malkia wa Waungama,
Malkia wa Mabikira,
Malkia wa Watakatifu wote,
Malkia uliyeumbwa, pasipo dhambi ya asili,
Malkia uliyepalizwa mbinguni,
Malkia wa Rozari takatifu,
Malkia wa amani.
Mwanakondoo wa Mungu, unayeondoa dhambi za dunia
Utusamehe Ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia
Utuhurumie Ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia
Utuhurumie Ee Bwana
K. Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu.
W. Tujaliwe ahadi za Kristu.
TUOMBE:
Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako tuwe siku zote na afya ya roho na ya mwili. kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakatifu, Bikra daima, tuopolewe na mashaka ya sasa, tupate furaha za milele. Kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.
KUMBUKA
Kumbuka, ee Bikira Maria mwenye rehema, haijasikilika kamwe kwamba ulimwacha mtu aliyekimbilia ulinzi wako, akiomba shime kwako, akitaka umwombee. Nami kwa matumaini hayo, nakukimbilia, ee Mama, mkuu wa mabikira; ninakuja kwako, nasimama mbele yako nikilalamika mimi mkosefu, ewe Mama wa Neno wa Mungu, usiyakatae maneno yangu, bali uyasikilize kwa wema, na unitimizie. Amina.
SALAMU MALKIA
Salamu, Malkia, Mama mwenye huruma; uzima, tulizo na matumaini yetu, salamu. Tunakusihi ugenini hapa sisi wana wa Eva. Tunakulilia tukilalamika na kuhuzunika bondeni huku kwenye machozi. Haya basi, Mwombezi wetu, utuangalie kwa macho yako yenye huruma. Na mwisho wa ugeni huu, utuonyeshe Yesu, mzao mbarikiwa wa tumbo lako. Ee mpole, ee mwema, ee mpendevu, Bikira Maria.
K. Utuombee, Mzazi mtakatifu wa Mungu.
W. Tujaliwe ahadi za Kristu.
Tuombe:
Ee Mungu, makimbilio na nguvu yetu, uwaangalie kwa wema watu wanaokulilia; na kwa maombezi ya Bikira Maria mtukufu asiye na kosa, Mzazi wa Mungu, na ya Mtakatifu Yosefu, mchumba wake, na ya Watakatifu Petro na Paulo Mitume wako, na ya Watakatifu wote: usikilize kwa huruma na wema sala tunazokutolea kwa wongofu wa wakosefu na kwa uhuru na utukufu wa Kanisa, mama mtakatifu. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.
Comments
Post a Comment
Thanks for Commenting at Visiontanzania, Please Share These useful materials to your friendsππ
Asante,
Regards,
System Administrator,
Visiontanzania,
+255747787796
+255673787796