Sala ya Usiku
SALA YA USIKU
Kwa jina la Baba..
Sala ya Kushukuru
Tunakushukuru, ee Mungu, kwa mapaji yote uliyo tujalia leo. Amina.
Tunakushukuru, ee Mungu, kwa mapaji yote uliyo tujalia leo. Amina.
Baba yetu
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
Salamu Maria
Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina
Sala ya Imani
Mungu wangu, nasadiki maneno yote linayosadiki, na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma: kwani ndiwe uliyefumbulia hayo, wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina.
Sala ya Matumaini
Mungu wangu, natumaini kwako nitapewa kwa njia ya Yesu Kristu, neema zako duniani na utukufu mbinguni, kwani ndiwe uliyeagana hayo nasi, nawe mwamini. Amina.
Sala ya Mapendo
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote; kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.
Sala ya kutubu
Mungu wangu, nimetubu sana dhambi zangu, kwani ndiwe mwema ndiwe mwenye kupendeza, wa- chukizwa na dhambi. Basi sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi. Amina.
Tuwaze katika moyo wetu makosa ya leo tuliyomkosea Mungu kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo, na kwa kutotimiza wajibu. (Subiri kidogo)
Nakuungamia Mungu Mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutotimiza wajibu, nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndiyo maana nakuomba Maria mwenye heri, Bikira daima, Malaika na Watakatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa Bwana Mungu wetu.
Mungu Mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu, atufikishe kwenye uzima wa milele. Amina.
Sala ya kuwaombea watu
Mungu wangu, nawaombea watu wa nchi hii, wapate kusikia maneno yako na kukupenda wewe Bwana Mungu wetu.
Kusifu
Malaika Mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili.
Malaika wa Bwana...Baba yetu... Salamu Maria...
Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu. Kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele Amina.
Enyi, Yesu, na Maria na Yosefu, nawatolea moyo na roho, na uzima wangu!
Enyi, Yesu, na Maria, na Yosefu, nijilieni saa ya kufa kwangu!
Enyi, Yesu, na Maria, na Yosefu, mnijalie nife mikononi mwenu!
Kwa heri Yesu, mpenzi mwema,
Nakwenda siudhike mno.
Nakushukuru, nakupenda,
Kwa hizo nyimbo za mwisho.
Asubuhi nitarudi.
Yesu kwa heri.
Kwa heri Mama mtakatifu,
Sasa napita pumzika.
Asante kwa moyo na nguvu,
Leo, umeniombea.
Asubuhi nitarudi.
Mama kwa heri.
Kwa heri Yosefu mnyenyekevu,
Kazi zatimilizika.
Kama mchana, leo usiku
Nisimamie salama.
Asubuhi nitarudi.
Yosefu kwa heri.
Comments
Post a Comment
Thanks for Commenting at Visiontanzania, Please Share These useful materials to your friendsππ
Asante,
Regards,
System Administrator,
Visiontanzania,
+255747787796
+255673787796