Novena kwa Mtakatifu Anthony wa Padua
NOVENA YA KUSALI KWA SIKU 9
Mtakatifu Anthony wa Padua, ninaweka (Taja nia ya Novena yako) chini ya ulinzi wako wenye nguvu. Kwa njia ya maombezi yako, kupitia Roho Mtakatifu nijalie mwanga, nguvu, akili na unyenyekevu ili niweze kupata mahitaji yangu ninayoomba kwa imani kuu kwa sala hii.
Ninakuomba Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na vitu vyote unijalie uwezo, ufahamu sahihi, na vipaji halisi katika maisha yangu. Amina.
NOVENA KWA MT. ANTHONY WA PADUA
SIKU YA 1 - 9
Ee mtakatifu Anthony, mnyenyekevu katika watakatifu, upendo wako kwa Mungu na ukarimu kwa viumbe vyake umekufanya kustahilishwa ukiwa duniani kupokea nguvu ya miujiza. Miujiza ilisubiri neno lako, ambalo daima ulikua tayari kuliongea kwa wale waliokuwa katika hofu na matatizo. Kwa kutiwa moyo na wazo hili ninakuomba uweze kupatiwa hitaji ninaloomba katika novena hii. (Taja hitaji lako)
Jibu la ombi langu huenda likahitaji muujiza, hata hivyo wewe ni mtakatifu wa miujiza. Ee Mtakatifu na mnyenyekevu Mt. Anthony, ambaye daima moyo wako ulikuwa umejawa na huzuni ya kibinadamu.
Ninakuomba umnong'oneze mtoto Yesu ombi langu katika sikio lake, ambaye daima alikubali kupokelewa katika mikono yako na shukrani ya moyo wangu itakuwa daima juu yako.
Baba yetu...
Salamu Maria...
Atukuzwe Baba...
Salamu Maria...
Atukuzwe Baba...
Mt. Anthony wa Padua... Utuombee
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumieKristo utuhurumie
Bwana utuhurumieBwana utuhurumie
Kristo utusikieKristo utusikilize
Utuhurumie
Roho Mtakatifu Mungu,Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu mmoja
Utuhurumie
Utuombee
Mt. Anthony wa Padua, Utuombee
Mt. Anthony nguzo ya wosia wa Mt. Fransisko, Utuombee
Mt. Anthony hekalu la hekima ya Mbinguni, Utuombee
Mt. Anthony mharibu wa ubatili wa dunia, Utuombee
Mt. Anthony aliyeshinda katika utakatifu,
Mt. Anthony mfano wa nyenyekevu,
Mt. Anthony mpenda msalaba,
Mt. Anthony mfiadini wa tamaa,
Mt. Anthony aliyejawa ukarimu,
Mt. Anthony mpenda haki,
Mt. Anthony tishio kwa wasiomwamini Kristo,
Mt. Anthony mfano wa ukamilifu,
Mt. Anthony mfariji wa wanaoteseka,
Mt. Anthony mrudisha vilivyopotea,
Mt. Anthony mlindaji wa wale walioonewa,
Mt. Anthony mfungua wafungwa,
Mt. Anthony muongoza wahujaji,
Mt. Anthony mrudisha afya,
Mt. Anthony mtenda miujiza,
Mt. Anthony mrudisha sauti iliyopotea,
Mt. Anthony mfungua viziwi,
Mt. Anthony mfukuzaji wa shetani,
Mt. Anthony mrudisha uhai,
Mt. Anthony mfukuza hofu,
Mt. Anthony mfano wa nyenyekevu,
Mt. Anthony mpenda msalaba,
Mt. Anthony mfiadini wa tamaa,
Mt. Anthony aliyejawa ukarimu,
Mt. Anthony mpenda haki,
Mt. Anthony tishio kwa wasiomwamini Kristo,
Mt. Anthony mfano wa ukamilifu,
Mt. Anthony mfariji wa wanaoteseka,
Mt. Anthony mrudisha vilivyopotea,
Mt. Anthony mlindaji wa wale walioonewa,
Mt. Anthony mfungua wafungwa,
Mt. Anthony muongoza wahujaji,
Mt. Anthony mrudisha afya,
Mt. Anthony mtenda miujiza,
Mt. Anthony mrudisha sauti iliyopotea,
Mt. Anthony mfungua viziwi,
Mt. Anthony mfukuzaji wa shetani,
Mt. Anthony mrudisha uhai,
Mt. Anthony mfukuza hofu,
Kutoka katika mitego ya shetani,
Utuopoe Ee Mt. Anthony
Kutoka katika radi na mafuriko,
Utuopoe Ee Mt. Anthony
Kutoka katika mitego ya shetani,
Utuopoe Ee Mt. Anthony
Kutoka katika radi na mafuriko,
Utuopoe Ee Mt. Anthony
Kutoka katika maovu ya roho na mwili,
Utuopoe Ee Mt. Anthony,
Kwa njia ya maombi yako,
Utuopoe Ee Mt. Anthony
Katika maisha yetu yote,
Mt. Anthony utulinde
Mwanakondoo wa Mungu, unayeondoa dhambi za dunia
Utusamehe Ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia
Utuhurumie Ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia
Utuhurumie Ee Bwana
Mt. Anthony wa Padua,
Utuombee tupate kujaliwa ahadi za Kristo.
Tuombe
Ee Mungu, ninakuomba kwa njia ya Mtakatifu Anthony wa Padua, muungamishi na mlinzi ulipe kanisa furaha, ili liweze daima kuimarishwa kwa njia ya maisha yake ili liweze kupata tuzo la milele kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina
__________________________________________________________
MT. ANTHONY WA PADUA
Mtakatifu wa miujiza
Mtakatifu wa miujiza
Comments
Post a Comment
Thanks for Commenting at Visiontanzania, Please Share These useful materials to your friendsππ
Asante,
Regards,
System Administrator,
Visiontanzania,
+255747787796
+255673787796