Sala kwa Mt. Anthony wa Padua
SALA YA KUTAFUTA KITU KILICHOPOTEA
Ee Mtakatifu Antoni wa Padua, uliye mpole kati ya watakatifu wote. Upendo wako kwa Mungu na kwa binadamu wakati ulipoishi hapa duniani, umetustahilia uwezo wa kutenda miujiza mingi kwa ajili ya wale wenye shida.
Kwa hiyo sisi pia tunapata moyo wa kukimbilia kwako na kuomba msaada wako. (Taja mahitaji yako) Labda ombi letu haliwezi kutimizwa bila mwujiza, hata hivyo je, huitwi Mtakatifu wa miujiza?
Kwa hiyo Mtakatifu Antoni wa Padua mwenye upole na huruma sana kwa watu wenye shida, sikiliza maombi yangu na kuyapeleka mbele ya Mtoto Yesu aliyependa kukaa mikononi mwako.
Nasi tutakuonyesha shukrani kubwa katika maisha yetu yote. Amina
Baba yetu...
Salamu Maria...
Atukuzwe Baba...
Salamu Maria...
Atukuzwe Baba...
Mt. Anthony wa Padua... Utuombee
__________________________________________________________
MT. ANTHONY WA PADUA
Mtakatifu wa miujiza
Mtakatifu wa miujiza
Comments
Post a Comment
Thanks for Commenting at Visiontanzania, Please Share These useful materials to your friendsππ
Asante,
Regards,
System Administrator,
Visiontanzania,
+255747787796
+255673787796