Sala ya asubuhi

 SALA YA ASUBUHI
Ee Baba yetu Mungu mkuu, 
Umenilinda usiku huu. 
Nakushukuru kwa moyo, 
Ee Baba, Mwana na Roho. 
Nilinde tena siku hii, 
Niache dhambi, nikutii.
Naomba sana, Baba wee 
Baraka yako nipokee. 
Bikira safi, Ee Maria, 
Nisipotee nisimamie, 
Mlinzi mkuu malaika wee. 
Kwa Mungu wetu niombee, 
Nitake, nitende mema tu 
Na mwisho nije kwako juu. Amina.


Nia njema

Kumheshimu Mungu wangu 
Namtolea roho yangu, 
Nifanye kazi nipumzike 
Amri zake tu nishike. 
Wazo, neno, tendo lote 
Namtolea Mungu pote 
Roho, mwili, chote changu, 
Pendo na uzima wangu 
Mungu wangu nitampenda,
Wala dhambi sitatenda. 
Jina lako nasifia, 
Utakalo hutimia. 
Kwa utii navumilia, 
Teso na matata pia. 
Nipe, Bwana, neema zako, 
Niongeze sifa yako. Amina.

Sala ya Matoleo
Ee Yesu, kwa mikono ya Bikira Maria, na kwa maungano na Sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, masumbuko na furaha zangu zote za leo. Ee Yesu, ufalme wako utufikie.

Baba yetu
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.

Salamu Maria
Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

Kanuni ya Imani
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, mwumba mbingu na dunia. Na kwa Yesu Kristu, Mwanaye wapekee, Bwana wetu; aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsio Pilato, akasulibiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka katika wafu; akapaa mbinguni; amekaa kuume ka Mungu Baba Mwenyezi; toka huko atakuja kuwahu kumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, uzima wa milele. Amina.

Amri za Mungu
1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine.
2. Usilitaje bure jina la Mungu wako.
3. Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4. Waheshimu baba na mama, upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue.
6. Usizini.
7. Usiibe.
8. Usiseme uwongo.
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya mtu mwingine.

Amri za Kanisa
1. Hudhuria Misa takatifu Dominika na sikukuu zilizoamriwa. 
2. Funga siku ya Jumatano ya Majivu, usile nyama siku ya Ijumaa Kuu.
3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka. 
4. Pokea Ekaristi takatifu hasa wakati wa Pasaka.
5. Saidia Kanisa katoliki kwa zaka.
6. Shika sheria katoliki za ndoa.

Sala ya Imani
Mungu wangu, nasadiki maneno yote linayosadiki, na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma: kwani ndiwe uliyefumbulia hayo, wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina.

Sala ya Matumaini
Mungu wangu, natumaini kwako nitapewa kwa njia ya Yesu Kristu, neema zako duniani na utukufu mbinguni, kwani ndiwe uliyeagana hayo nasi, nawe mwamini. Amina.

Sala ya Mapendo
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote; kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.

Sala ya kutubu
Mungu wangu, nimetubu sana dhambi zangu, kwani ndiwe mwema ndiwe mwenye kupendeza, wa- chukizwa na dhambi. Basi sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi. Amina.

Sala kwa Malaika Mlinzi
Malaika Mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili.


Malaika wa Bwana
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria.
Naye akapata mimba kwa Roho Mtakatifu. 
Salamu, Maria, ...

Ndimi mtumishi wa Bwana.
Nitendewe ulivyonena.
Salamu, Maria,...

Neno la Mungu akatwaa mwili.
Akakaa kwetu.
Salamu, Maria,...

Utuombee, Mzazi mtakatifu wa Mungu.
Tujaliwe ahadi za Kristu.

Tuombe
Tunakuomba, Ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu kwa mateso na msalaba wake tufikishwe kwenye utukufu na ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.

Malkia wa mbingu
Malaika wa mbingu, furahi, Aleluya,
Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya,

Amefufuka alivyosema, Aleluya.
Utuombee kwa Mungu, Aleluya.

Furahi, shangilia, ee Bikira Maria, Aleluya,
Kwani hakika Bwana amefufuka, Aleluya.

Tuombe
Ee Mungu, uliyependa kuifurahisha dunia kwa kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristu, Mwanao: Fanyiza, twakuomba, kwa ajili ya Bikira Maria, tupate nasi furaha za uzima wa milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.

Asanteni kwa kuwa nasi. Mtangulize Mungu kwa kila jambo lako. Hapa chini ni sala muhimu, bonyeza tu. 
πŸ’  SALA YA ASUBUHI
πŸ’  SALA YA USIKU
πŸ”ΉπŸ”ΉπŸ”Ή
Usisite kutuandikia hapo chini (Enter Comment) maoni yako, umejifunza nini, umefurahishwa na kipi au una mapendekezo gani kwa #visiontanzania.....
πŸ”ΉπŸ”ΉπŸ”Ή

♂️MENU

Comments

Popular Visiontanzania Posts

KIJANA MIAKA 18-35 USIKOSE HII

ACADEMY MEMBERSHIP ONLINE APPLICATION For VISION ENTREPRENEURSHIP ACADEMY

MENU

NGUZO KUU 8 ZA MAFANIKO KATIKA JAMBO LOLOTE

MFAHAMU FLAVIANA MATATA MPAMBANAJI TOP

HISTORIA YA SAID SALM BAKHRESA

MAMBO YALETAYO FURAHA YA KWELI MAISHANI

FUNZO KUU LA KUFANIKIWA ATOA JACK MA

NJIA RAHISI YA KUISHI NDOTO ZAKO