Matendo ya rozari Takatifu

MATENDO / MAFUNGU YA ROZARI TAKATIFU
MATENDO YA FURAHA 
Jumatatu na Jumamosi

Tendo la kwanza
Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. 
Tumwombe Mungu  atujalie unyenyekevu.

Tendo la pili
Maria anakwenda kumtembelea Elizabeti.  
Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.

Tendo la tatu
Yesu anazaliwa Betlehemu.  
Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara. 

Tendo la nne
Yesu anatolewa hekaluni.  
Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.

Tendo la tano
Maria anamkuta Yesu hekaluni.  
Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.


MATENDO YA UCHUNGU 
Jumanne na Ijumaa

Tendo la kwanza
Yesu anatoka jasho la damu.  
Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.

Tendo la pili
Yesu anapigwa kwa mijeledi.  
Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.

Tendo la tatu
Yesu anatiwa miiba kichwani. 
Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.

Tendo la nne
Yesu anachukua Msalaba.  
Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.

Tendo la tano
Yesu anakufa Msalabani. 
Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.


MATENDO YA UTUKUFU 
Jumatano na Jumapili

Tendo la kwanza
Yesu anafufuka.  
Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.

Tendo la pili
Yesu anapaa mbinguni. 
Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.

Tendo la tatu
Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. 
Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.

Tendo la nne
Bikira Maria anapalizwa mbinguni. 
Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.

Tendo la tano
Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni.  
Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.


MATENDO YA MWANGA 
Alhamisi

Tendo la kwanza
Yesu anabatizwa Mto Jordani. 
Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.

Tendo la pili
Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana.  
Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya injili.

Tendo la tatu
Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. 
Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli. 

Tendo la nne
Yesu anageuka sura. 
Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.

Tendo la tano
Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristi.  
Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.

Asanteni kwa kuwa nasi. Mtangulize Mungu kwa kila jambo lako. Hapa chini ni sala muhimu, bonyeza tu. 
πŸ’  SALA YA ASUBUHI
πŸ’  SALA YA USIKU
πŸ”ΉπŸ”ΉπŸ”Ή
Usisite kutuandikia hapo chini (Enter Comment) maoni yako, umejifunza nini, umefurahishwa na kipi au una mapendekezo gani kwa #visiontanzania.....
πŸ”ΉπŸ”ΉπŸ”Ή

♂️MENU

Comments

Popular Visiontanzania Posts

KIJANA MIAKA 18-35 USIKOSE HII

ACADEMY MEMBERSHIP ONLINE APPLICATION For VISION ENTREPRENEURSHIP ACADEMY

MENU

NGUZO KUU 8 ZA MAFANIKO KATIKA JAMBO LOLOTE

MFAHAMU FLAVIANA MATATA MPAMBANAJI TOP

HISTORIA YA SAID SALM BAKHRESA

MAMBO YALETAYO FURAHA YA KWELI MAISHANI

FUNZO KUU LA KUFANIKIWA ATOA JACK MA

NJIA RAHISI YA KUISHI NDOTO ZAKO